Mzunguko wa 23 wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) unaanza leo kwa mechi mbili kupigwa katika viwanja tofauti, na zote zitakuwa mbashara kupitia Azam TV.
Katika Dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza, Mbao FC watakuwa wenyeji wa Lipuli FC kutoka mkoani Iringa, mchezo utakaokuwa mbashara Azam Sports 2 kuanzia saa 10:00 jioni.
Kuelekea katika mchezo huo, Kikosi cha Lipuli FC kiliwasili salama jijini Mwanza usiku wa kuamkia jana tayari kuwavaa wapinzani wao hao huku Kocha wa Lipuli FC, Selemani Matola akitamba kuibuka na ushindi katika mchezo huo licha ya kuwakosa nyota wake muhimu Adam Salamba na Steve Maganga ambao wana kadi mbili za njano.
Mchezo mwingine unapigwa katika Dimba la Namfua mjini Singida ukiwakutanisha wenyeji Singida United na wakata miwa wa Mtibwa Sugar na utakufikia mbashara kupitia Azam TWO kuanzia saa 10:00 jioni.
No comments:
Post a Comment