TUMUSIFU BWANA

prop

Monday, 2 April 2018

Tetesi za soka na usajili barani uraya jumanne 3.04.2018

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba amesema hana tatizo na meneja Jose Mourinho na hafikirii kuihama klabu hiyo. Hii ni licha ya Mfaransa huyo wa miaka 25 kuwa akiwekwa benchi mechi za karibuni. (Telefoot kupitia Manchester Evening News)
Everton, West Ham na Swansea wote wanamtaka mshambuliaji wa Mali anayechezea Porto Moussa Marega, 26. (Mirror)
Meneja wa zamani wa Chelsea Gianluca Vialli amesema meneja wa sasa wa klabu hiyo Antonio Conte bila shaka anasubiri sana kuondoka. (Sky Italia kupitia Metro)
Conte anasema hana wasiwasi kuhusu mustakanali wake kama meneja Chelsea baada ya klabu hiyo kulazwa 3-1 na Tottenham na kudidimiza matumaini ya klabu hiyo kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao. (Guardian)

Alexis Sanchez na Paul Pogba
Taarifa zinazomhusisha fowadi wa Brazil mwenye miaka 26 Neymar na kuhamia Real Madrid ni "uvumi usio na msingi" kwa mujibu wa mchezaji mwenzake Paris St-Germain Kylian Mbappe. (Telefoot via Goal)
Beki wa miaka 24 kutoka Ufaransa anayechezea Barcelona Samuel Umtiti ambaye amehusishwa na kuhamia Manchester United, anasema hali kwamba kifungu cha kumfungua kutoka kwa mkataba wake klabu hiyo si cha juu sana inamtia wasiwasi. Hata hivyo, amesema ametosheka kusalia katika klabu yake PSG
 Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero atakuwa amepata nafuu vya kutosha kuweza kuwa kwenye benchi mechi ya mkondo wa kwanza robofainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Liverpool. 

No comments:

Post a Comment