Matokeo Simba vs Prisons VPL 16 April 2018
Matokeo Ya Mchezo kati ya Simba dhidi Ya Tanzania Prisons mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Vodacom Premier League uwanja wa Taifa Jijini Dar Es Salaam.
>> Soma habari za Simba Hapa <<
Timu ndiyo zinaingia uwanjani zikitokea Vyumbani, Simba wamevaa tshirts nyekundu na Bukta zao ni Nyeupe.
Wakati Prisons wamevaa Kijani Tshirts na Bukta za Kijani Pia
Mwamuzi wa kati ni Shomari Lawi kutoka Mwanga Kigoma.
Tayari timu zote zipo kwenye Uwanja na Muda wowote mechi Itaanza
Mechi Imeanza katika uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam
Dakika ya kwanza SImba wanapata Kona
Kona inashindwa kuwa na madhara yoyote Langoni mwa Tanzania Prisons Kipa Aron Anadaka
Dakika ya 4 Timu zinacheza kwa Kusomana matokeo yakiwa bado ni tasa
Dakika ya 7 Mohammed Rashid alijaribu kuchomoka lakini akawekwa chini na Juuko Murshid, Inapigwa Faulo mabeki wa Simba wanaondoa mpira kwenye hatari
Dakika 10
Simba 0 – 0 Prisons
Dakika ya 11 Simba wanapata Kona, Inapigwa na Shomari Kapombe lakini Kipa wa Prisons anadaka mpira Huo
Dakika 15
Simba 0 – 0 Tanzania Prisons
Dakika ya 17 Simba wanapata Kona ya Tatu
Kona inapigwa na Kichuya mabeki wanaokoa na Kuondoa mpira kwenye eneo la hatari, Bado 0 kwa 0
Dakika ya 20 Offside John Bocco mara baada ya Kupenyezewa mpira na Shiza Kichuya
Dakika ya 22 Simba wawanapata Kona ya 4 lakini haina madhara kwa Prisons.
Simba wanapata tena Kona Hii ni ya Tano matokeo yakiwa 0 kwa 0
Dakika ya 23 Eliuta Mpepo anajaribu kupiga Shuti linaenda pembeni ya Lango la Simba
Dakika ya 27 Mpira Unachezwa zaidi katikati ya Uwanja wanachofanya walinzi wa Prisons ni kutibua Mipira Ya Simba huku wao wakitegemea kucheza mipira Mirefu
Dakika ya 32 Shomari Kapombe anamimina Krosi safi beki wa Prisons anatoa inakuwa kona ya 6 kwa Simba.
Inapigwa Kona inatoka Nje.
Simba 0 – – Prisons
Simba wanapata Kona Mbili mfululizo, Wanakuwa na Kona nane mpaka sasa Prisons hawana kona hata Moja
Goaaaaaaaaaaal dakika ya 35 Nahodha John Bocco anaipatia Simba bao la Kuongoza.
Ulipigwa Mpira na Erasto Nyoni kutokea Pembeni ikaenda ikagonga mwamba wa pembeni ukarudi uwanjani na Bocco akapigwa Kichwa Kikazama golini.
Dakika 40
Simba 1 – 0 Bocco
No comments:
Post a Comment