Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Rais John Magufuli amefanya uteuzi wa Majaji 10 wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Naibu Mkurugenzi wa Mashitaka, Wakili Mkuu wa Serikali na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu Jijini DSM imesema Majaji walioteuliwa na Rais John Magufuli ni Elvin Mugeta, Elinaza Luvanda, Yose Mlyambina, Immaculata Banzi na Mustafa Siyani. Majaji wengine ni Paul Ngwembe, Agnes Mgeyekwa, Stephen Magoiga, Thadeo Mwenempazi na Butamo Philip.
Aidha Rais Magufuli amemteua Dokta Evaristo Longopa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Edson Makallo kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashitaka, Dokta Julius Mashamba kuwa Wakili Mkuu wa Serikali na Dokta Ally Possi kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.
prop
Sunday, 15 April 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment