Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
SERIKALI imeendelea kuwasisitiza waajiri wote nchini, kuzingatia muda wa unyosheshaji watoto uliotolewa kwa watumishi wa umma, mashirika na sekta binafsi.
Pia imewataka watumishi wote waliokutana na vikwazo katika utekelezaji wa suala hilo, kutoa taarifa. Akizungumza na gazeti hili jana, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema watumishi watakaokuwa na malalamiko ya kutendewa kinyume ya agizo hilo, waripoti katika ofisi yake au katika ofisi za wakurugenzi wa halmashauri.
Julai mwaka jana, serikali kupitia wizara hiyo ilitoa agizo lililowataka waaajiri wote kutenga muda wa saa 2 kila siku, baada ya kumaliza miezi mitatu ya likizo ya uzazi, kwa watumishi hao kwenda kunyoshesha ili kuwezesha watoto kuwa na afya bora inayotokana na maziwa ya mama. “Niendelee kusisitiza juu ya suala hili kuwa agizo hilo linapaswa kutekelezwa kikamilifu kwa kuwa ni wajibu wa kila mama kumnyonyesha mtoto bila kumpa chakula kingine chochote katika kipindi cha miezi sita, nasisitiza kuwa hili ni agizo na linapaswa kutekelezwa,” alisema Ummy.
Alisema hapendi kusikia kuwa kuna mwajiri yoyote anakiuka agizo hilo, huku akiwataka watendaji wa umma, mashirika na taasisi zote kuzingatia suala hilo katika kutambua umuhimu wa mama mzazi kunyonyesha kwa muda uliowekwa kwa kipindi chote cha miezi sita. Alisema takwimu zinaonesha kuwa asilimia 11 ya watoto wenye umri chini ya miezi sita, wamekuwa hawanyonyeshwi ipasavyo na badala yake wazazi wa watoto hao, wamekuwa wakiwachanganyia watoto hao vyakula mbalimbali au vimiminika wakiamini kuwa ni stahiki kwao.
Ummy pia alisema asilimia nne ya watoto hao wanapewa maziwa mengine tofauti na mama zao, yakiwemo ya unga au mifugo huku asilimia mbili wanalishwa vinywaji ambavyo havina maziwa. Alisema kuwa ni gharama kubwa katika kuhudumia watoto walio na utapiamlo, tatizo ambalo moja ya sababu zake ni pale mtoto anapokosa maziwa ya mama kwa muda mrefu na kwamba ili kumuepusha na hali hiyo, njia rahisi ikiwemo kutengwa kwa masaa hayo zinahitajika.
Katika maelezo yake hayo ya awali, Waziri Ummy alisema kuwa endapo suala la lishe litazingatiwa vyema na wadau wote, kwa kiasi kikubwa litaweza kuwaondoa watoto katika utapiamlo linalosababisha baadhi ya watoto kudumaa kiakili. Kutokana na hatua hiyo baadhi ya wadau, kikiwemo Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA), waempongeza Waziri Ummy kutokana na hatua hiyo kwa kusema kuwa hiyo ni hatua muhimu kwa ajili ya ustawi wa mtoto ambayo kwa namna nyingine inachangia maendeleo ya Taifa.
TAWLA imesema hatua hiyo ni jambo jema, kwa kuwa imeonesha ni kwa namna gani ambavyo serikali inaona umuhimu wa suala la unyonyeshaji wa mtoto kwa lengo la kuboresha afya yake, hivyo linapaswa kuungwa mkono na wadau wote hususani waajiri. Katika maelezo yake hayo ya awali, Waziri Ummy alisema kuwa endapo suala la lishe likizingatiwa vyema na wadau wote, kwa kiasi kikubwa litaweza kuwaondoa tatizo la utapiamlo kwa watoto, linalosababisha baadhi yao kudumaa kiakili.
prop
Monday, 19 March 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment