TUMUSIFU BWANA

prop

Thursday, 22 March 2018

Selikali ya amuonya diamond platinamu

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo nchini Tanzania imemshutumu nwanamuziki maarufu Diamond Platnumz kwa kauli aliyoitoa kuhusu kufungiwa kwa nyimbo zake mbili.
Waziri Dkt Harrison Mwakyembe amesema "amesikitishwa" na kauli alizozitoa mwanamuziki huyo akihojiwa na kituo kimoja cha redio jijini Dar es Salaam.
Waziri huyo amesema maamuzi ya kuzifingia baadhi ya nyimbo na wasanii wawili kwa kukiuka maadili yalifanywa kwa mujibu wa sheria na siyo kwa utashi wa Naibu Waziri Juliana Shonza.
Mwanamuziki huyo wa kizazi kipya, ambaye jina lake halisi ni Nassib Abdul, anadaiwa kumlaumu naibu huyo wa waziri.
"Diamond atambue kuwa serikali ina taratibu zake na maamuzi ya naibu waziri ni maamuzi ya wizara," Dkt Mwakyembe amenukuliwa kwenye taarifa iliyotumwa na wizara hiyo kwa vyombo vya habari.
Nyimbo za Diamond zilizofungiwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) mwishoni mwa mwezi uliopita ni Hallelujah (uliomshirikisha Morgan Heritage ) na Waka Waka (uliomshirikisha Rick Ross).
Nyimbo za Diamond na wengine zafungiwa Tanzania
Kikwete: Viongozi wa upinzani sio maadui wa serikali Afrika
Waziri huyo alisema kuna vikao vingi vya wasanii ambavyo vimekuwa vikifanywa kati ya serikali na wasanii "lakini Diamond hakuwahi kuhudhuria vikao hivyo."
"Si wajibu wa serikali kumfanyia kikao cha peke yake."
"Sheria ni ya watu wote bila kujali umaarufu au nafasi ya mtu katika jamii, hivyo msanii Diamond anapaswa kutii sheria na mamlaka zilizowekwa."
Waziri huyo alimwambia mwanamuziki huyo kwamba si busara kwake kushindana na serikali na kwamba endapo ana ushauri wowote, ni vyema kwake kuuwasilisha kwa njia sahihi "lakini si kwa kumshambulia waziri kwa dharau na kejeli kama alivyofanya."

No comments:

Post a Comment