TUMUSIFU BWANA

prop

Tuesday 27 March 2018

Ronardo apigwa stop ureno vs uholanzi 0_3

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Mabingwa wa Ulaya Ureno walipokezwa kichapo cha kushangaza na Uholanzi katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyochezewa mjini Geneva, Uswizi.
Winga wa zamani wa Manchester United Memphis Depay na mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Ryan Babel waliwaweka Waholanzi 2-0 mbele.
Jedwali la Msimamo wa ligi ya EPL 2017/18
Beki wa Uholanzi Virgil van Dijk, ambaye majuzi alitawazwa nahodha mpya wa timu hiyo, alifunga la tatu.
Mchezaji wa Ureno Joao Cancelo alipewa kadi nyekundu dakika ya 61 baada ya kupokezwa kadi ya pili ya manjano.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Cristiano Ronaldo alikuwa amefunga mabao mechi nane mfululizo kabla ya mechi hiyo
Katika mechi hiyo, mkimbio wa kufunga mechi nane mtawalia wa mshambuliaji nyota wa Ureno anayechezea Real Madrid Cristiano Ronaldo ulifikishwa kikomo.
Nahodha huyo wa Ureno aliondolewa uwanjani dakika ya 68 na nafasi yake akaingia kiungo wa Monaco Joao Moutinho.
Shujaa wa Panama anayepanga kuhangaisha England Kombe la Dunia
Ronaldo alikuwa amefunga mabao 17 akichezea Real na mawili akichezea Ureno dhidi ya Misri Ijumaa katika kipindi hicho alichofunga mabao mechi nane mtawalia.

No comments:

Post a Comment