Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Mkutano huo na wataalamu wa kisheria ukiendelea.
JOPO la Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Maofisa Ustawi wa Jamii, Wanasheria pamoja na askari Polisi kutoka Dawati la Jinsia wamemuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, kuwa wamejidhatiti vyema kuwasikiliza akinamama waliotelekezwa na hawapatiwi pesa ya matunzo ya mtoto kwenye zoezi la siku tano za kuwapatia msaada wa kisheria linalotaraji kuanza Aprili 9 mwaka huu.
Akizungumza na wataalamu hao leo, Makonda amesema tatizo la wamama waliotelekezwa ni kubwa na limekuwa likisababisha kinamama na watoto kuishi maisha ya tabu na kusababisha ongezeko la watoto wa mitaani na vizazi vya watoto wenye chuki na baba zao.
Makonda amesema lengo la zoezi hilo sio ugomvi bali ni kumwezesha mtoto kupata mahitaji ili aweze kuitumia vyema fursa ya elimu bure chini ya serikali ya awamu ya tano.
Aidha Makonda amewahimiza wataalamu hao kuhakikisha wanawasikiliza kinamama kwa umakini na kusimamia haki pasipo upendeleo.
Pamoja na hayo amesema wapo wakinababa ambao wameanza kutoa fedha za matunzo ya mtoto baada ya kusikia tangazo ambapo amewasihi akinamama waliotelekezewa watoto kufika Aprili 9 mwaka huu ili kuonana na wataalamu waweke makubaliano kwenye mfumo rasmi wa kimaandishi.
prop
Tuesday, 27 March 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment