Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Dube.
VIDOLE viwili vimekandamiza tundu mbili za pua. Nalazimika kufanya hivyo kutokana na harufu kali ya moshi mzito unaotokana na kuvutwa kwa ile sigara kubwa. Yes, ni ule mmea wa Jamaica, wenye matawi na majani yaliyotawanyika. Mmeshanielewa bwana!
Ghafla kwa mbali, nasikia korasi ya wimbo uitwao The Way It Is; “Be good to the people running your way up the ladder, cause you will need them on your way down.”
(Kuwa mwema kwa watu unapokuwa kwenye harakati za kufikia vilele mbalimbali vya mafanikio, kwa sababu ipo siku utawahitaji watu wakati wa kushindwa kwako).
Bado ninatafakari nini cha kufanya, hapohapo harufu ya mmea inakata na sauti nzito yenye kukwaruza inasikika, ikiniuliza mimi ni nani, natazama kwa umakini na kubaini mtu huyo ni aliyekuwa nguli wa muziki wa Rege, marehemu Lucky Philip Dube ambapo mazungumzo yetu yanafanyika kwa Lugha ya Kiingereza na hapa nimeyatafsiri ili tuwe pamoja, teremsha macho;
LUCKY DUBE: Unajua una bahati sana hadi kufika eneo hili ukiwa hai, huko nje hujakutana na walinzi? Hili eneo ni hatari sana kwa wageni, haya niambie wewe ni nani na unataka nini?
MIMI: Naitwa Masalu, ni mwandishi wa habari kutoka nchini Tanzania, nimefurahi kukutana na wewe na ninaomba tuzungumze tu.
LUCKY DUBE: (huku akitingisha rasta zake na kunikazia macho), unataka tuzungumzie nini, mbona tunataka kuchoshana asubuhi yote hii? Haya ninakusikiliza basi.
MIMI: Kwanza ninakupongeza kwa umahiri uliokuwa nao kwenye utunzi, uandishi na uimbaji wa mashairi yako, hakika nyimbo zako haziwezi kuchuja.
LUCKY DUBE: Unafahamu nyimbo zangu kweli wewe? Hebu nitajie japo tano tu ndipo tuanze mazungumzo.
MIMI: (haraka sana tena kwa kujiamini mno), kuna The Way It Is, Remember Me, The Prisoner,…
LUCKY DUBE: Hapo sawa, unajua niliondoka duniani katika mazingira ambayo hadi leo huwa nabaki najiuliza sababu ni zipi.
MIMI: Nakumbuka ulipigwa risasi usiku na watu wasiojulikana, nje
ya nyumba yako wakati ukitoka matembezini, hivi ilikuwaje?
Diamond.
LUCKY DUBE: Wewe kweli ni mwandishi, japo sijakuomba hata kitambulisho, lakini huo ndiyo ukweli, siku hiyo nimetoka zangu kwenye misele, tena nilikuwa nimeshafika nje ya geti la nyumba yangu kabisa, nikashtukia milio ya risasi na mwanzo sikujua kama ilikuwa inanilenga mimi, niliona ni kitu cha kawaida kwa sababu masuala ya bastola kule Sauzi (Afrika Kusini) ni kama samaki na maji.
MIMI: Mmh, ikawaje?
LUCKY DUBE: Nilikuwa nimesahau rimoti ya kufungulia geti, nikashuka ili nijikague vizuri, ni hapo ndipo nilifanya kosa, zilimiminika risasi kama mvua, iliyoniondoa kabisa dunia ni ile iliyopenya shingoni na kutokea upande wa pili, yaani ililenga koromeo, giza nene lilitanda na hapohapo nikajikuta nipo huku, dah! (anainama na ghafla machozi yanaanza kumchuruzika bila kutoa sauti ya kilio).
MIMI: Pole sana. Kwani unadhani sababu za wewe kushambuliwa kwa risasi ni nini?
LUCKY DUBE: Kama nilivyosema hapo awali, hakika huwa sijui hadi leo. Wakati mwingine huwa nawaza labda ni uhasama wa kikazi kutoka kwa wanamuziki wenzangu au watu tu wenye wivu, lakini huwa sipendi kumhisi mtu yeyote.
MIMI: Haya maisha haya! Hivi
inakuwaje mtu unamuua mwenzako kama unachinja kuku? Hadi unashika bunduki na kufyatua kiwambo, moyoni haushtakiwi na nafsi? Hatupaswi kuuana namna hiyo, mwenye mamlaka na uhai wa binadamu ni Mungu pekee, lakini kila anayeua kwa upanga, naye atauawa kwa upanga au na wewe uliwahi kuua huko nyuma au kutuma watu wamuue mtu?
LUCKY DUBE: (kwa mshtuko na hamaki kubwa), unasema nini wewe? Nimefanya kosa kukukubalia kufanya mahojiano? Basi ondoka bwana, siwezi kufanya unyama wa namna hiyo, mimi huyu niue? Umenikosea sana bwana.
MIMI: Nimeuliza tu. Basi nisamehe.
LUCKY DUBE: Sawa, jana kulikuwa na tamasha rasmi la wanamuziki kutoka Tanzania, wakawa wanamtaja sana mtu anaitwa Diamond kwamba siku hizi ndiye nembo ya Tanzania akishindana sijui na Ali nani, nimesahau.
MIMI: Ali Kiba.
LUCKY DUBE: Kitu kama hicho, lakini kilichosemwa kuhusu Diamond sikukipenda kabisa na ninataka nimshauri
prop
Wednesday, 21 March 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment