TUMUSIFU BWANA

prop

Monday, 19 March 2018

Kemikali inayo otesha matiti kwa wanaume

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
husiano kati ya matiti yasio ya kawaida ambayo humea miongoni mwa wavulana na utumizi wa mafuta ya mti wa lavender na ule wa chai umetoa uzito tofauti baada ya utafiti kubaini kwamba kemikali nane zinazopatikana katika mafuta ya miti hiyo uharibu kazi ya homoni za kiume.
Utafiti huo wa Marekani umebaini kwamba kemikali muhimu katika mafuta hayo hupiga jeki homoni za kike na kuharibu homoni za kiume.
Mafuta ya mimea hiyo hupatikana katika bidhaa tofauti kama vile sabuni, mafuta ya kujipaka mafuta ya kuosha nywele pamoja na na bidhaa za kutengeza nywele.
Pia ni maarufu sana katika bidhaa za kuosha mbali na matibabu. Kiongozi wa utafiti huo, J.Tyler Ramsey kutoka taasisi ya kitaifa kuhusu mazingira ya sayansi ya afya katika jimbo la Carolina Kaskazini alionya watu kutahadhari wakati wa utumizi wa mafuta hayo.
''Jamii yetu huona mafuta hayo ya asilia kuwa salama. Hatahivyo humiliki kiwango kikubwa cha kemikali na ni sharti yatumiwe na tahadhari kwa kuwa baadhi yao husababisha uharibifu wa homoni''.
Visa kadhaa vya tatizo la kumea matiti miongoni mwa wanaume vimeripotiwa kutokana na utumizi wa mafuta hayo yenye manukato.
Baada ya kusitisha utumizi wa mafuta hayo tatizo hilo huisha lenyewe. Utafiti wa awali uliofanywa na Daktari Kenneth Korach - ambaye alichunguzwa kutokana na utafiti huo ulibaini kwamba mafuta ya mti wa Lavender na ule wa chai ulikuwa na ishara za kuharibu homoni zinazodhibiti tabia za kiume ambazo zinaweza kuathiri kubalehe na ukuwaji.

No comments:

Post a Comment