Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Chama kinachotawala nchini Kenya, Jubilee, kilisema Jumanne kwamba kiliilipa kampuni iitwayo SLC, iliyo na uhusiano na kampuni ya Cambridge anlytica (CA), inayogubikwa na utata, kukifanyia matangazo na kukitafutia umaarufu wakati wa kampeni za chaguzi kuu mbili zilzizopita.
Naibu mwenyekiti wa chama hicho cha Jubilee, David Murathe, alikiri kwamba kampuni hiyo ilihusika kukitafutia umaarufu chama hicho lakini hakutoa maelezo ya kina kuhusu mbinu zilizotumika.
Cambridge Analytica inashutumiwa kwamba ilihusika kwenye mzozo ambao pia unaikumba pia kampuni ya mtandao ya Facebook.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, CA ilichangia pakubwa ushindi wa rais Donald Trump kwenye uchaguzi wa Novemba mwaka wa 2016.
Kampuni hiyo imehiusishwa na kashfa zingine mbalimbali, kikiwa ni pamoja na kuwatumia makahaba kwenye baadhi ya michakato.
Facebook tayari imeikataza CA kutumia mtandao huo kwa matangazo yake.
Shirika la habari la Channel 4 news la Uingereza, lilionyesha video iliyorekodia kwa siri, na kufichua kwamba kampuni hiyo ilihusika pakubwa kwenye kampeni za chaguzi mbili za Kenya, za mwaka 2013 na 2017, chini ya ufadhili wa muungano wa kisisa wa wakati huo uliopewa jina la 'Jubilee'.
Afisa mkuu wa Cambridge Analytica alisimamishwa kazi siku ya Jumanne kufuatia kashfa hiyo.
prop
Tuesday, 20 March 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment