Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Ibrahim Ajib na Mbwana Samatta katika mazoezi ya Taifa Stars.
Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga bado hajaweka wazi wazi kikosi chake cha kwanza lakini kwa mujibu wa mazoezi yake tayari ameshapata kikosi cha wachezaji wa kwanza.
Taifa Stars imekuwa ikifanya mazoezi ya katika uwanja wa Taifa kujiandaa na mechi za kirafiki dhidi ya Botswana na Burundi siku ya Jumamosi na Jumapili.
Mayanga amekuwa akiwagawa wachezaji katika makundi mawili. Kundi la kwanza linaonekana kuwa ndio litaunda kikosi cha kwanza huku wale kundi la pili wakihitaji kumshawishi zaidi.
Mayanga anaonekana kusuka kikosi kipya japo umuhimu wa kusaka ushindi unamlazimisha kuwajumlisha baadhi ya wakongwe kama Erasto Nyoni katika maeneo ambayo bado hakuna mbadala imara.
Kundi la kwanza linamjuisha Aishi Manula ambaye ana nafasi kubwa ya kucheza mechi yake ya tatu mfululizo akilinda lango la Taifa Stars na kumweka benchi mkongwe Deogratius Munishi.
kikosi kipya cha SalumMayanga kitakuwa hivi:
Aishi Manula ( kipa ),
Mabeki wa pembeni : Mohamed Hussein, Shomari Kapombe
Hassan Ramadhan naye amejumuishwa katika kundi la kwanza.
Mabeki wa kati: Abdi Banda, Erasto Nyoni
Kiungo wakabaji: Himid Mao
Kiungo wa Kushambulia: Frank Domayo
Kiungo wa kulia: Simon Msuva
Kiungo wa Kushoto: Shiza Kichuya
( Hii ilikuwa ni kabla ya Farid Mussa kuanza mazoezi )
Washambuliaji wa Kati: Mbwana Samatta, Ibrahim Ajib
prop
Thursday, 22 March 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment