Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
England watakapoingia wuanjani dhidi ya limbukeni Panama katika michuano ya Kombe la Dunia uwanjani Nizhny Novgorod mnamo 24 Juni, itakuwa ni karibu miaka miwili tangu waliponyenyekezwa na taifa jingine linaloibuka katika soka - Iceland.
Iceland walipata ushindi uwanjani Nice katika michuano ya Euro 2016 kutokana na unyonge wa England na kuchipuka kwa wachezaji wenye vipaji hatua iliyomfanya meneja Roy Hodgson kujiuzulu baada ya miaka minne
Nchini Urusi, England watakutana na taifa jingine lisilofahamika sana kwa soka ambalo litakuwa linamtegemea sana mchezaji mkabaji ambaye amejizolea sifa si haba.
Roman Torres ni beki wa kati wa miraba minne ambaye hupendwa sana Panama, kiasi cha kuchukuliwa kama nyota wa filamu.
Panama - na Torres - walifikaje hapa? Ni tishio kiasi gani kwa England? siku moja katika jiji la Panama City, mji mkuu wa taifa hilo la Amerika ya Kati, akiwa na beki huyo anayechezea klabu ya Seattle Sounders.
prop
Monday, 26 March 2018
Beki wa panama Roman Torres kuiongoza timu yake kombe la dunia zidiya england urusi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment