Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
BARAZA la Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wametoa waraka mzito wa Sikukuu ya Pasaka ambao umesainiwa na maaskofu 27 waliokutana Machi 15, 2018 na umepangwa kusomwa kesho Machi 25, 2018 katika makanisa yote nchini.
Katika ujumbe huo maaskofu, wamegusia masuala makuu matatu ambayo ni jamii na uchumi, maisha na siasa na mambo mtambuka yanayohusiana na hayo ikiwemo demokrasia, huku wakisisitiza Katiba mpya ya wananchi ni suluhu ya yote. Pia, masuala ya wanasiasa kuhama chama kimoja na kwenda kingine pamoja na mabadiliko ya mara kwa mara ya mfumo wa elimu kwamba una athari kwa Taifa.
UJUMBE WA PASAKA KUTOKA BARAZA LA MAASKOFU WA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA (KKKT)
TAIFA LETU, AMANI YETU
A. UTANGULIZI
“Fumbua Kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu; Uwatetee watu wote walioachwa peke yao; Fumbuakinywa chako, uhukumu kwa haki; uwapatie maskini na wahitaji haki yao”(Mithali31:8-9).
Wapendwa wana KKKT,
Watukuka, watu wote na familia ya Mungu katika Taifa letu, “Amani iwe kwenu!; Kristo Amefufuka (Yohana 20:19).
Bwana wetu Yesu Kristo mfufuka, alipowatokea wanafunzi wake wakiwa wamejifungia ndani kwa hofu ya Wayahudi, aliwasalimu na kujifunua kwao kwa salaamu ya kuwatakia amani. Wapendwa watu wa Mungu, katika umoja wetu, sisi maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), tunawasalimuni nyote kwa kuwatakia amani. Bwana wetu Yesu Kristo Amefufuka kweli kweli – Haleluya!.
Yeye ni amani yetu, na pia ni amani kwa watu wote wenye mapenzi mema. Kwa kufufuka kwake, upendo umeishinda chuki; unyenyekevu umeushinda ubabe; nuru imelishinda giza; haki imeshinda udhalimu; msamaha umeshinda visasi; ujasiri umeshinda hofu; na kwa hiyo uzima umeshinda kifo.
Mwaka 2017, Kanisa letu limeadhimisha miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa. Tukiwa wana Matengenezo tumekumbushwa tena kuwa mwanadamu anaokolewa kwa Neema ya Mungu tu: Wokovu Hauuzwi; Mwanadamu Hauzwi walakununuliwa; na Uumbaji hauuzwi. Kanisa zima na dunia kwa ujumla tunaitwa kusimama pamoja na kuueleza ukweli huu unaoziweka huru dhamiri zetu (Yohana 8:31-32).
Matengenezo (Reforms) ni dhana ya kibiblia. Tangu zama za Agano la Kale, Mungu kwa nyakati mbalimbali aliteua wajumbe wake kuwasilisha ujumbe wake kwa jamii na kwa watawala wa dunia. Kwa Umungu wake, aliwainua wanawake na wanaume kwa makusudi ya kutoa unabii yaani, ujumbe wa Mungu kwa jamii au watawala. Wakati mwingine aliinua manabii kuwasemea wasiokuwa na sauti. Unabii na Matengenezo ni njia ya Mungu katika kusimika utawala wa haki na unaostawisha uhuru na amani.
Kwa namna ya pekee, manabii kama Daniel, walionya juu ya uongozi unaojenga uhalali wake katika wingi wa watu wanaokubaliana na uongozi huo hata kama ni katika makosa. Haikuwa rahisi kibinadamu kuukosoa mfumo kama huo lakini Mungu alitumia manabii kuzungumza na mfumo wa namna hiyo.
Unabii wa Daniel 3:7 unasema, “Kwa hiyo watu WOTE,mara waliposikia sauti za baragumu, filimbi, kinubi, zeze, santuri, zumari, na sauti za ala nyingine za muziki,walianguka kifudifudi na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebkadneza aliisimamisha”.
Hapa tunaona kosa la kiongozi kutengeneza sanamu, linasababisha kosa la watu wanaokubali kuiabudu hiyo sanamu. Tumetafakari na kusadiki kuwa, kosa la kiongozi au mfumo, haliwaondolei hatia wanaomfuata kiongozi au kuufuata mfumo, hata kama watu hao walikula kiapo cha kutii maongozi ya kiongozi huyo na mfumo wake.
Mbele ya Mungu hakuna ile kanuni ya kuwajibika kwa pamoja. Kila mtu kwa dhamiri yake anawajibika mbele za Mungu. Kwa upande mwingine, pamoja na uwajibikaji wa mtu binafsi, Nabii Ezekieli anatukumbusha na kutuonya kuwa tusipoonya na kusimama katika zamu yetu, hatia na damu ya wasio na hatia, itadaiwa mikononi mwetu (Ezekiel 33: 8-9).
Adhimisho la kufufuka kwa Yesu Kristo (Pasaka) na maadhimisho ya miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa, yanatusukuma kutafakari utume wa Kanisa katika jamii kwa nyakati zetu. Tunaalikwa kupeleka ujumbe wa amani kwa watu wote na kusimama kwa ujasiri
prop
Saturday, 24 March 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment