TUMUSIFU BWANA

prop

Thursday, 22 March 2018

Asilimia 53 vijijini, 78 mijini wanapata maji

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
WAKATI leo ikiadhimishwa Siku ya Maji Duniani, takwimu zinaonesha asilimia 53.1 ya watu wanaoishi vijijini wanapata maji, wakati mijini ni asilimia 78. Pia imeeleza kuwa serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji imefanya juhudi kadhaa ili kufanikisha mpango wa upatikanaji wa maji kwa wote kama ilivyoainishwa kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochambuliwa na kutolewa na Taasisi ya WaterAid Tanzania, Tanzania imepiga hatua kwa zaidi ya miaka 15 iliyopita kupitia Mpango wa Serikali wa Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP), hususani mijini, licha ya idadi ya watu kuongezeka huku uhitaji wa maji safi ukiongezeka.

Mkurugenzi wa WaterAid Tanzania, Dk Ibrahim Kabole, alieleza hali ya upatikanaji maji nchini akisema kuwa, kuna hatua kubwa imepigwa na kwamba, upatikanaji wa maji safi na salama unaenda sambamba na muda uliopangwa na hivyo, kutoa unafuu kwa wananchi.

Alisema: “Wizara ya Maji na Umwagiliaji, mapema mwezi huu ilitueleza kuwa serikali imepiga hatua na kwamba asilimia 53.1 ya watu wanaoishi vijijini wanapata maji, na vilevile asilimia 78 kwa upande wa mijini wanapata huduma hiyo muhimu.”

Akaongeza, “hii ni hatua kubwa na yenye kuonesha mwelekeo mzuri, kama hatua imepigwa kwenye mpango wa miaka 15 kwenye sekta ya maji, ni wazi kuwa kuna unafuu wananchi wanaupata licha ya kuwa idadi yao imeongezeka.”

UCHUMI WA KUTEGEMEA MAJI

Kuhusu uchumi wa Tanzania, huku akiihusisha Ripoti ya Benki ya Dunia Novemba mwaka jana, Kabole alisema Tanzania ina uchumi unaokua kwa kasi, hivyo pasipo kuboresha kwa haraka jinsi inavyoweza kusimamia maji yake, itakuwa vigumu kuhimili ukuaji huo.

Ripoti hiyo ilisema kuwa ongezeko la idadi ya watu nchini linachangia kuongezeka kwa mahitaji ya maji na kusababishaTanzania kuwa moja ya nchi zenye uhitaji wa maji.

AFYA YA WANANCHI

Katika uchambuzi wake, Mkurugenzi huyo alisema ripoti ya mpango wa pamoja wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) unaonesha kuwa asilimia 37 ya Watanzania wanategemea vyanzo vya maji visivyo salama, hivyo kuna hatari ya kuongezeka kwa magonjwa yanayohusu maji kama vile kipindupindu.

Ripoti ya UNICEF ya mwaka 2011, inaonesha kuwa takribani asilimia 70 ya matumizi ya sekta ya afya hutumika kutibu magonjwa yanayohusu maji kwa gharama ya dola za Marekani zaidi ya milioni 500 kiasi ambacho kingeweza kuwekezwa mahali pengine kwa ajili ya kukuza uchumi.

Alisema kitendo cha serikali kuongeza kasi na kuboresha upatikanaji wa maji, kitasaidia kufikia malengo mengine ya kitaifa kwa kuwa maji ni muhimu kwa afya, elimu, uchumi na usawa wa kijinsia.

Akasema: “Kuna baadhi ya changamoto zilizotajwa kuathiri sekta ya maji ikiwemo fedha, uendelevu na mabadiliko ya hali ya hewa. Lakini, kama kutakuwa na njia mbadala za maji kufikia wananchi, basi serikali itamfikia kila mtu, kila mahali.”

Mkurugenzi huyo alisema serikali inahitaji kuwa na teknolojia ya gharama nafuu ili jamii ziweze kudumisha mifumo ya maji, na pia kuwapo uwajibikaji zaidi kwa mambo ya fedha ili fedha zinazopatikana kutokana na huduma za maji, zitumike katika ukarabati wa miradi hiyo. Alisema ushirikiano uliopo kati ya serikali, sekta binafsi, taasisi za elimu na washirika wa maendeleo ni muhimu katika kumfikia kila mmoja, kila mahali katika suala la maji ifikapo mwaka 2030.

MAFANIKIO NA MKAKATI WA SERIKALI Serikali imesema kutokana na kuongezeka kwa Watanzania na kufikia milioni 53, kila Mtanzania anaweza kutumia maji kwa mita za ukubwa 1,500 kwa mwaka tofauti na kipindi ambacho nchi ilipata uhuru maana kila Mtanzania aliweza kutumia mita za ukubwa 8,000 kwa mwaka.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwelwe alisema hayo juzi jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa mkakati wa Benki ya Dunia wa namna uwepo wa maji safi na salama unavyopunguza viashiria umasikini, ikiwa ni utekelezwaji wa mpango wa maendeleo endelevu (SDGs).

Kuhusu uhitaji wa maji, Waziri Kamwelwe ali

No comments:

Post a Comment