TUMUSIFU BWANA

prop

Sunday, 18 March 2018

ANAYE TARAJIA KUSHINDA URAIS RUSIA

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
  
Wananchi wa Urusi wanaendelea kupiga kura Jumapili katika uchaguzi mkuu wa urais ambapo hakuna shaka Rais aliyeko madarakani Vladimir Putin ataendelea kushikilia madaraka na urais. Putin ameongoza taifa la Urusi kwa miaka 18.
Hata hivyo kiongozi huyo anakabiliwa na changamoto kadhaa lakini hakuna upinzani wa kutisha kutoka kwa wanaogombea naye. Kila mmoja kati ya wanaogombea wengine– akiwemo supasta na mwengine mwenye kupigania utaifa kwanza- wanatarajiwa kupata kura chache mno.

Putin anatarajiwa kupata kura zaidi ya asilimia 50 katika uchaguzi huo, lakini timu yake ya uchaguzi inamatarajio ya kukusanya kura asilimia 70.

Uchaguzi wa Jumapili unafanyika katika nyakati 11 tofauti, ukianza na mashariki ya mbali na kumalizika na wilaya ya Kaliningrad. Takriban watu milioni 109 wameandikishwa kupiga kura. Shirika la serikali linaloendesha uchaguzi linatarajia asilimia 71 ya watu hao waliojiandikisha kuja kupiga kura.

Ingawaje, Kituo cha kitafiti cha shirika la kiraia Levada kimefanya utafiti Disemba 2017 na utafiti huo unaonyesha asilimia 58 ya wapiga kura walikuwa wamepanga kususia uchaguzi huo.

Hasimu wa Putin kisiasa ambaye ni kiongozi wa chama cha upinzani Alexei Navalny aliyekuwa ni tishio kubwa kwa Putin ametolewa katika kinyang’anyiro hicho cha urais baada ya kukutwa na hatia ya ubadhirifu Disemba 2017.

Baada ya kupewa kifungo mbadala cha miaka mitano, amesema kuwa hukumu hiyo ya mahakama ilikuwa inamsukumo wa kisiasa, ili kumuondoa katika mbio hizo za uchaguzi.

Navalny anaongoza juhudi za kususia uchaguzi, wakati waandaaji wa uchaguzi wa Urusi wanategemea wapiga kura wengi zaidi kuhalalisha uchaguzi ambao kwa muda mrefu unadaiwa umeshaamuliwa.

No comments:

Post a Comment