TUMUSIFU BWANA

prop

Sunday 6 May 2018

Matokeo ya mechi ya simba vs Ndanda fc may 6.2018

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Matokeo Simba vs Ndanda 6 May 2018

Matokeo ya Moja kwa Moja Simba dhidi ya Ndanda kutoka Mtwara, Simba sc Inaongoza Ligi wakati huo Ndanda wanakomaa kuhakikisha hawashuki daraja.

Lakini katika historia mechi 7 ambazo zimewahi kuikutanisha Ndanda na Simba, Simba kashinda mechi zote.

Timu zinatoka Vyumbani na Kuingia uwanjani

Mwamuzi ni Erick Onoka  kutoka Mkoani Arusha

Mechi Imeanza

Simba 0 – 0 Ndanda

Dakika ya 2 Mpaka sasa Ndanda wamepiga Shuti moja langoni mwa Simba.

Dakika ya 3 Simba wanapata Kona, Inapigwa Kona Fupi inakosa madhara langoni mwa Ndanda

Dakika ya 4 Faulo ya Kichuya Inazaa kona kwa Simba lakini bado haina madhara

Dakika 5

Simba 0 – 0 Ndanda

Dakika ya 9 Simba wanakosa nafasi Okwi anakosa mpira Wa Kichwa

Dakika 15

Simba 0 – 0 Ndanda

Dakika ya 15 Simba wanacheza kona Nyingine, Magoli yangekuwa Kona basi Simba wanatatu wakati huo Ndanda hawana kitu

Ndanda wanatulia na Kupiga pasi kadhaa dakika ya 19 wanapata Kona.

Hakuna faida kwa Kona yao

Dakika ya 20 Nicolas Gyan anawekwa chini karibu na Kibendera, Faulo kuelekea Ndanda

Dakika ya 22 John Bocco aliingia kwa kasi langoni mwa Ndanda beki anajitutumua na Kuutoa Nje.

Dakika ya 23 Shiza Kichuya anazungusha MPIRA unagonga Mwamba Unarudi ilikuwa ni baada ya Kona Fupi

Dakika ya 26 Okwi anatandika shuti kipa anatoa na kuwa Kona

Dakika ya 27

Simba 0 – 0 Ndanda
Dakika 30

Simba 0 – 0 Ndanda

Dakika ya 36 Omary Mponda akiwa kwenye nafasi nzuri anapiga mpira Fyongo, Bado 0 kwa 0

Dakika ya 37 Kona nyingine kwa Simba, Ni Kona ya 6 kwa Simba, ndanda wanakona moja.

Dakika ya 43 Mwenye uwanja wake Emmanuel Okwi anaipatia Simba bao

Simba 1 – 0 Ndanda

Dakika 3 zimeongezwa kufidia dakika zilizopotea Kipindi cha Kwanza

No comments:

Post a Comment