Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Haji Manara apewa Onyo kali na TFF,Mwenyewe afunguka haya
Shirikisho la soka Nchini TFF kupitia Bodi ya Ligi Tanzania Premier League Board (TPLB) imempa Onyo kali Afisa habari wa klabu ya Simba kutokana na Kitendo chake cha Kuingia uwanjani mara baada ya mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga jumapili iliyopita.
Barua Hiyo inaelezea kuwa kitendo alichofanya Manara ni kinyume na Kanuni namba 14 (11) Ambayo inazuia mtu ambaye si mhusika kuingia uwanjani kabla, wakati na baada ya mchezo.
Hata hivyo Haji Manara mwenyewe msomaji wa Kwataunit.com kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ujumbe wa Kutaka RADHI kutokana na Kitendo Hiko.
” Muungwana akivuliwa nguo huchutama..naomba radhi bodi ya ligi,TFF na wadau wote..nilihemewa na furaha ndugu zangu..hakuna raha kwangu mm na kwa mshabiki kama kumgalagaza mtani…it will never happen again..ila sijui itakuwaje siku ya kukabidhiwa mwali😁😁😁 @tanfootball #bodiyaligi 🙏🙏 “
prop
Thursday, 3 May 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment