TUMUSIFU BWANA

prop

Thursday, 19 April 2018

TETESI ZA USAJILI TANZANIA 19.2018

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
USAJILI: Yanga kumsajili Rasta Msumbufu wa Welayta Dicha Djako Arafat,Ishu kamili hii hapa

Baada ya Kuonyesha uwezo wa Hali ya Juu kwenye michezo miwili kati ya Yanga na Waethiopia Welayta Dicha mchezaji Djako Arafat kuna taarifa za Kuaminika kuwa tayari ameingia kwenye Rada za Mabingwa wa Tanzania Yanga.

Mara baada ya Mchezo kati ya Yanga na Welayta Dicha Nchini kumalizika Djako alionekana kuwakona baadhi ya Viongozi na washabiki wa Yanga, Lakini kwa mara nyingine jana akicheza huko Ethiopia na Yanga akazidi kuikuna kamati ya Usajili klabu ya Yanga.

Baada ya mchezo wa Jana ambao Djako Arafat ndiye aliyefunga bao la Welayta Dicha  mapema Tu katika dakika ya Pili akitumia makosa ya walinzi wa Yanga waliozubaa kuondoa Mpira wa Kona Kamati ya usajili ya Yanga ikiongozwa Na Hussein Nyika ilionekana kumfata Djako ambaye alivaa jezi namba 10 akiwa na rasta Kichwani na Kuonekana kuzungumza Naye.

HAIJAISHIA HAPO.

Leo kupitia kwa moja kati ya Maafisa habari wa Yanga Godlisten Anderson maarufu zaidi kama Chicharito kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika Ujumbe unaoashiria kuwa mchezaji huyo muda tu ndo usubiriwe kwa yeye kuvaa uzi wa Yanga.

Kupitia Ukurasa wa Instagram wa Chicharito amepost video ambayo inaonekana baadhi ya Viongozi wa kamati ya Usajili klabu ya Yanga wakimshika Mkono na Kuonekana kuongea na Djako Arafat.

No comments:

Post a Comment