Matokeo mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara Vodacom Premier League katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya kati ya Mbeya City dhidi Ya Singida United
>> Soma habari za michezo hapa <<
Mechi Imeanza katika uwanja wa Sokoine Mkoani Mbeya
Mbeya City 0 – 0 Singida United
Dakika ya 4 Free Kick ya Haruna Shamte inawatanguliza Mbeya City mbele kwa Bao 1.
Mbeya City 1 – 0 Singida United
Dakika ya 8 Frank Hamis Ikobela anajaribu kuingia katika ngome ya Mbeya City lakini Kipa Wa Singida United Manyika Peter Jr anawahi anadaka Mpira.
Dakika 10
Mbeya City 1 – 0 Singida United
Singida wanaonekana kutulia na Kupiga Pasi Fupi fupi
Dakika ya 15
Mbeya City 1 – 0 Singida United (4′ Haruna Shamte)
Dakika ya 16 Maliki Antiri anasawazisha bao kwa Singida United, Mambo ni sawa kwa sawa Sokoine yani 1 kwa 1.
Dakika ya 17
Mbeya City 1 – 1 Singida United
Dakika ya 21 Mbeya City wanapata Faulo nje kidogo ya 18
Anapiga Shamte lakini Kipa Manyika anapangua mpira uluiokuwa hatari langoni mwa Singida United
Dakika ya 26 Mbeya City wanakosa nafasi ya wazi
Dakika ya 28 Mpira wa adhabu unapigwa kuelekea Mbeya City, Unakosa madhara.
Dakika ya 30 Yusuph Kagoma anapewa kadi ya njano kwa kumchezea vibaya Frank Ikobela
Dakika ya 31 Mpira wa Hatari unapanguliwa na Manyika na Kuwa Kona
Inapigwa Kona Kennedy Juma anaondoa katika hatari
Mbeya City 1 – 1 Singida United
Dakika ya 38 Iddi Suleiman “Idd Nado” anachukua nafasi ya Victor Hangaya, Nado ndiye aliyesawazisha goli kwa Mbeya City ilipocheza na Yanga
Dakika ya 43 Iddy Nado anawekwa chini na Kaseke akielekea Golini.
Dakika ya 43 Inapigwa Free Kick tamu na Mwakatundu Manyika anatoa na Kuwa Kona.
Mbeya City 1 – 1 Singida United
HALF TIME
Mbeya City 1 – 1 Singida United
KIPINDI CHA PILI
Mechi inaendelea kwa kipindi cha Pili
Mbeya City 1 – 1 Singida United
Dakika ya 50 Bado ni 1 kwa 1
dakika ya 54 Deus Kaseke alijaribu kupiga Shuti linalopaa washabiki wa Mbeya City wanazomea
Dakika ya 59 Mbeya City wanakosa nafasi ya wazi, Eliud Ambokile anapishana na Mpira
Dakika ya 60 Eliud Ambokile kwa mara nyingine anawekewa Mpira na Frank Ikobela anapaisha akiwa yeye na Kipa
Mbeya City 1 – 1 Singida United
Dakika ya 61 Yusuph Kagoma anatoka anaingia Mudathir Yahya Abbas
Dakika ya 65
Mbeya City 1 – 1 Singida United
Dakika ya 69 Walitengeneza Shambulizi zuri Mbeya City anyika akawa shujaa
Dakika ya 77 Ametoka Salita Kambale ameingia Mundia
Mbeya City 1 – 1 Singida United
Dakika ya 80 bado ni 1 kwa 1
Dakika ya 88 timu zote zinaonekana kucheza kwa Tahadhari, Matokeo yakiwa bado 1kwa 1
FULL TIME
Mbeya City 1 – 1 Singida United (Haruna Shamte, Malik Antiri)
Matokeo Njombe Mji vs Ndanda 27 April 2018
Timu ya Njombe Mji ya Mkoani Njombe imefanikiwa kupata Ushindi wa bao 2 kwa 0 Ikicheza dhidi ya Ndanda uwanja wa sabasaba.
Bao la kwanza la Njombe Mji limepatikana kipindi cha Kwanza katika dakika ya 17 kupitia kwa Notiker Masasi na bao la Pili
No comments:
Post a Comment