Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Maafisa watatu wakuu wa tume ya uchaguzi nchini Kenya (IEBC) akiwemo naibu mwenyekiti wamejiuzulu wakidai kutokuwa jna imani na mwenyekiti wa tume hiyo, Wafula Chebukati.
Makamishna hao wamedai kuwa bodi hiyo imeshindwa kutimiza wajibu na imeeingiliwa na watu wengine.
Wakihutubia wanahabari jijini Nairobi, makamishna hao Consolata Nkatha, Paul Kurgat na Margaret Mwachanya wamedai kuwa Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati ameshindwa kuiongoza tume hiyo na kudai kwamba tume hiyo imeingiliwa na watu kutoka nje wanaoshawishi jinsi inavyofanya kazi.
Haki miliki ya pichaREUTERS
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Kenya Wafula Chebukati
''Kwa muda murefu sasa, mwenyekiti ameshindwa kutoa muongozo wa utaratibu kwa wakati mgumu na anapohitajika kufanya hivo.
Katika taarifa yake hivi punde kwa waandishi wa habari, mwenyekiti wa tume hiyo ya IEBC - Wafula Chebukati amesema kwamba hakujakuwa na mawasiliano rasmi kuhusu kujiuzulu kwa makamishna hao watatu na kwamba amepata kusikia kuhusu taarifa hiyo kupitia vyombo vya habari nchini.
prop
Monday, 16 April 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment