Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kudownload APP YETU BOFYA HAPA, Au ingia playstore tafuta KALAMBO NEWS kisha bofya install.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma atakabiliwa na kesi ya rushwa inayohusisha mkataba wa silaha wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 2.5 ambao ulisainiwa mwisho wa mwaka 1990, amesema mwendesha mashtaka mkuu Shaun Abrahams, Ijumaa.
“Baada ya kulipima suala hili, nafikiria kuna uwezekano mkubwa wa kufanikiwa kumshtaki Zuma kwa makosa yaliyo orodheshwa anayotuhumiwa kwayo,” amesema Abrahams.
Hata hivyo Zuma amekanusha tuhuma zote, amesema Abrahams.
Chanzo cha habari kimeripoti kuwa Zuma anatuhumiwa kutaka rushwa kwa nia ya kujinufaisha kifahari yeye binafsi.
Mshauri wake wa fedha wakati huo alikutwa na hatia ya kuomba rushwa hizo mwaka 2005 na Zuma alimfukuza kazi.
Zuma alifutiwa mashtaka hayo muda mchache kabla ya kuwa rais mwaka 2009.
prop
Saturday, 17 March 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment